
Dalili za mauaji ya kimbari Rwanda
Polisi nchini Zimbabwe, wanasema kuwa wameanzisha msako mkali
wa afisaa mmoja mkuu wa zamani nchini Rwanda ambaye anatuhumiwa kwa kuhusika na
mauaji ya Kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda.
Protais Mpiranya alikuwa kamanda wa ulinzi wa rais mwaka huo na anatuhumiwa
kwa kuhusika pakubwa na mauaji ya watutsi 800,000 pamoja na wahutu wenye msimamo
wa kadri. Makama maalum kuhusu mauaji wa kimbari nchini Rwanda imeahidi kumkabidhi zawadi ya dola milioni tano yeyote mwenye taarifa kumhusu Protais.
"Tunamtaka. Awe hai au akiwa amekufa. Tunatafuta taarifa kumhusu ili tumkamate.Hatufahamu mda ambao amekuwa akiishi hapa nchini'' alisema afisaa mkuu wa polisi Zimbabwe Peter Magwenzi.
Mwaka jana afisaa mmoja wa nchi hiyo alikana kuwa Zimbabwe inamhifadhi Protais.
No comments:
Post a Comment