Monday, September 10, 2012

Jeshi la Mali lauwa wasafiri


Jeshi la Mali linasema kuwa limewapiga risasi na kuwauwa watu 16 katika jimbo la Segou, katikati mwa nchi, baada ya gari la watu hao kutosimama kwenye kituo cha ukaguzi.
Rais Dioncounda Traore wa Mali (kulia) na Waziri Mkuu Midibo Diarra

Wakuu wanasema gari hilo liliendelea hata baada ya kuonywa kwa risasi.
Inaarifiwa kuwa baadhi ya wale waliouwawa ni wahubiri wa Kiislamu kutoka Mauritania, ambao walikuwa wakielekea kwenye mkutano wa kidini nchini Mali.
Waandishi wa habari wanasema huenda kuwa jeshi liliwafikiria wasafiri hao kuwa wapiganaji wa Kiislamu ambao wanadhibiti eneo la kaskazini mwa Mali

No comments:

Post a Comment