Friday, September 21, 2012

Mawaziri 6 wajiuzulu India

 

Mawaziri sita wa muungano tawala nchini India wamejiuzulu, kufuatia mipango ya serikali ya kuruhusu maduka makubwa ya kigeni kuendesha sekta ya bidhaa za reja reja nchini humo.
Duru zinaarifu kuwa uamuzi wa chama cha Trinamool Congress kikiongozwa na Mamata Banerjee,kutounga mkono muungano huo zinazidisha shinikizo za kisiasa ingawa hazitishii ushawishi wa chama cha serikali.
Waziri mkuu wa nchi hiyo, Manmohan Singh, anatarajiwa kutoa taarifa kupitia televisheni ya kitaifa kutetea sera zake kuhusu uwekezaji wa kigeni na kuondoa ruzuku ya mafuta.

No comments:

Post a Comment