Friday, September 21, 2012

KITCHEN PARTY YA WINNIE URASSA YAFANA DAR

 



Winnie akiwa amebebwa na wenzake wakati wa Kitchen Party yake iliyofanyika juzi katika Ukumbi wa Latino Bar, Tabata Aroma Septemba 16 mwaka huu.
Mashoga zake wakionesha mambo hadharani
Winnie akiaga baada ya shughuli kumalizika
Mmoja wa wageni waaalikwa akenda kumtunza winnie. PICHA ZOTE NA MDAU KHAMIS MUSSA

Mawaziri 6 wajiuzulu India

 

Mawaziri sita wa muungano tawala nchini India wamejiuzulu, kufuatia mipango ya serikali ya kuruhusu maduka makubwa ya kigeni kuendesha sekta ya bidhaa za reja reja nchini humo.
Duru zinaarifu kuwa uamuzi wa chama cha Trinamool Congress kikiongozwa na Mamata Banerjee,kutounga mkono muungano huo zinazidisha shinikizo za kisiasa ingawa hazitishii ushawishi wa chama cha serikali.
Waziri mkuu wa nchi hiyo, Manmohan Singh, anatarajiwa kutoa taarifa kupitia televisheni ya kitaifa kutetea sera zake kuhusu uwekezaji wa kigeni na kuondoa ruzuku ya mafuta.

Waziri mkuu mpya wa Ethiopia

Hailemariam Desalegn
Waziri mkuu mpya wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, ameapishwa kuchukua wadhifa wa hayati Meles Zenawi aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 21.
Mwingine aliyeapishwa ni naibu wake Demeke Mekonen, ambaye alikuwa anashikilia wadhifa wa waziri wa elimu.
 
Bwana Hailemariam Desalegn, amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa ana furaha kuchukua wadhifa huo na yuko tayari kufanya majukumu yake kwa kujitolea.
Hailemariam aliungwa mkono bila pingamizi na bunge la waakilishi ambalo lina wanachama wengi wa muungano tawala kuchukua wadhifa huo
Sherehe ya kumuapisha waziri mkuu huyo iliendeshwa na rais wa mahakama ya juu zaidi nchini humo, Tegene Getaneh na kuonyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa.
Hayati Zenawi alifariki mwezi jana mjini Brussels baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Julius Malema matatani kwa utata wake

 

Julius Maleme
Polisi wa Afrika Kusini wametoa waranti ya kukamatwa mwanasiasa wa Afrika kusini anayeleta utatanishi, Julius Malema, ambaye alifukuzwa kutoka chama tawala cha ANC.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani juma lijalo kuhusu mashtaka ya ku-ghu-shi fedha, rushwa, na wizi kwa njia za udanganyifu.
Kamati maalumu ya uchunguzi, iitwayo "the Hawks", imekuwa ikichunguza shughuli za kibiashara za Bwana Malema.
Bwana Malema, ambaye aliwahi kuwa mfuasi mkubwa wa Rais Jacob Zuma, amegombana na washirika wake wa zamani, na akafukuzwa chamani, kwa kutoa wito kuwa serikali ya Botswana inafaa kupinduliwa.

Thursday, September 20, 2012

HIVI NDIVYO MPENDWA WETU DAUD MWANGOSI ALIVYOAGA DUNIA KWA KUULIWA KIKATILI

 




Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi

Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini


Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari


JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.

Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.

" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza

Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.

"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.

Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.

Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .

Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.

"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.

Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .
MWISHO

SIMBA YAIGAGADUA JKT RUVU 2-0 UWANJA WA TAIFA

 

Mchezaji Nassor Masoud 'Cholo' wa Simba, akipambana na Amos Mgisa wa JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba imeshinda mabao 2 - 0. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Mwinyi Kazimoto wa Simba, akimtoka Stanlay Nkomola wa JKT Ruvu katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Stanlay Nkomola wa JKT Ruvu, akimkata Mwinyi Kazimoto wa Simba katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Mchezaji Mrisho Ngassa wa Simba, akijaribu kumtoka Stanlay Nkomola wa JKT Ruvu wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mrisho Ngassa wa Simba, akipambana na Ramadhan Kauga wa JKT Ruvu wakati wa mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Mchezaji Damas Makwaya wa JKT Ruvu, akijaribu kuuondoa mpira miguuni mwa Amir Maftah wa Simba katika mchezo huo.

Mchezaji Mrisho Ngassa wa Simba, akijaribu kumpita Stanlay Nkomola wa JKT Ruvu wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


Mchezaji Daniel Akuffor wa Simba, akipasua katikati ya wachezaji wa JKT Ruvu, wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Emmanuel Okwi akipiga mpira kuelekea lango la JKT Ruvu, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu hizo, Uwanja wa Taifa, dar es Salaam leo.


Mashabiki wa Simba, wakifurahia timu yao, wakati wa mchezo dhidi ya JKT Ruvu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


Mashabiki wa Simba, wakifurahia mchezo wa timu yao dhidi ya JKT Ruvu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Daniel Akuffor wa Simba (kushoto), akimpongeza mwenzake, Amri Kiemba baada ya kumpatia pasi aliyomalizia kwa kufunga goli la kwanza kwa timu yao ya Simba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Nassor Chollo wa Simba, akimtoka Said Otega wa JKT Ruvu.

Wachezaji wa Simba wakimpongeza Haruna Moshi (chini) wa timu hiyo, baada ya kuipatia timu yake bao la Pili katika mchezo huo.

Mrisho Ngassa wa Simba (aliyefichika) na Ramadhan Kauga wa JKT Ruvu, wakipambana wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


Mrisho Ngassa wa Simba (aliyefichika, jezi nyekundu) na Ramadhan Kauga wa JKT Ruvu, wakipambana wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


Hadi mwisho wa mchezo huo, ubao wa matokeo ulikuwa ukionesha Simba 2, JKT Ruvu 0.

Bernard Membe holds a meeting with the Head of EUCAP NESTOR



Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister of Foreign Affairs and International Co-operation today met with Real Admiral Launey, Head of EUCAP Nestor in his office in Dar es Salaam. The two discussed about the launch of a comprehensive regional training mission which aims at strengthening the maritime capacities of countries in the Horn of Africa and the Western Indian Ocean.
Hon. Membe (2nd right) explains about piracy situation in the Indian Ocean. Listening is Real Admiral Launey (2nd left), Head of EUCAP Nestor, Ambassador Filiberto Ceriani Sebregondi (2nd left), Head of Delegation of the European Union, and Ambassador Dora Msechu, Director of the Department of Europe and Americas in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.
Ambassador Sebregondi (left), explains EUCAP Nestor's objectives that includes strengthening the sea going maritime capacity of countries such as Kenya, Tanzania, Seychelles and Djibouti and a vision to strength the Rule of Law sector in Somalia, by providing training of a land-based coastal police force.
A photo of the Tanzania delegation that included Hon. Membe (left), Ambassador Msechu (2nd left), Mr. Togolani Mavura, Personal Assistant to Hon. Membe, Mr. Frank Mhina, Desk Office of European Union affairs in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.
A photo of the European Union delegation led by Real Admiral Launey (right). Others are Ambassador Sebregondi (2nd right), Ms. Natasha Hryckow (2nd left), Head of Country Mission Kenya and Mr. Thomas Wiersing (left), Operations Unit (Civilian Planning and Conduct Capabilities).
A group photo of Hon. Membe in a meeting with European Union delegation and Tanzania delegation during their meeting at the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.
Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister of Foreign Affairs and International Co-operation chats briefly with Head of Delegation of the European Union, Ambassador Filiberto Ceriani Sebregondi, before saying goodbye.
Hon. Membe saying goodbye to Real Admiral Launey of EUCAP Nestor. All photos by Tagie Daisy Mwakawag-Tanzania's Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation

Zimbabwe inamsaka mshukiwa wa Rwanda

Dalili za mauaji ya kimbari Rwanda
Polisi nchini Zimbabwe, wanasema kuwa wameanzisha msako mkali wa afisaa mmoja mkuu wa zamani nchini Rwanda ambaye anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya Kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda.
Protais Mpiranya alikuwa kamanda wa ulinzi wa rais mwaka huo na anatuhumiwa kwa kuhusika pakubwa na mauaji ya watutsi 800,000 pamoja na wahutu wenye msimamo wa kadri.
Zimbabwe imekuwa ikishutumiwa kwa kumpa hifadhi afisaa huyo wa zamani.
Makama maalum kuhusu mauaji wa kimbari nchini Rwanda imeahidi kumkabidhi zawadi ya dola milioni tano yeyote mwenye taarifa kumhusu Protais.
"Tunamtaka. Awe hai au akiwa amekufa. Tunatafuta taarifa kumhusu ili tumkamate.Hatufahamu mda ambao amekuwa akiishi hapa nchini'' alisema afisaa mkuu wa polisi Zimbabwe Peter Magwenzi.
Mwaka jana afisaa mmoja wa nchi hiyo alikana kuwa Zimbabwe inamhifadhi Protais.

Makabiliano ya polisi na wachimba migodi

Wachimba migodi wakikabiliana na polisi
Polisi nchini Afrika Kusini wametumia risasi za mipira na gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wanagoma karibu na mgodi mmoja unaomilikiwa na kampuni ya Anglo American.
Makabiliano hayo yametokea siku moja baada ya mkataba kuafikiwa kati ya wachimba migodi wa Marikana na wamiliki wa kampuni ya Lonmin.
"hatutaruhusu mikutano yoyote haramu kufanyika'' alisema msemaji mmoja wa polisi.
Wafanyakazi wa kampuni ya Lonmin walisitisha mgomo wao wa wiki sita siku ya Jumanne baada ya kukubali nyongeza ya asilimia 22 ya mishahara.
Migomo hiyo ilisambaa hadi katika migodi mingine nchini humo. Afrika Kusini ni mojawapo ya nchi zinazozalisha madini mengi duniani.
Mnamo siku ya Jumatatu rais Jacob Zuma alisema kuwa migomo katika sekta ya madini ililetea nchi hiyo hasara ya zaidi ya dola nusu milioni.
Migomo ilianza nchini humo baada ya kampuni ya madini ya Anglo American Platinum (amplats),kampuni kubwa zaidi ya madini ya Platinum duniani kufungua kiwanda chake baada ya kufungwa wiki jana kufuatia migomo hiyo.
Msemaji wa kampuni ya Amplats, Mpumi Sithole alisema kuwa migodi ya Rustenburg,ambacho ni kitovu cha uchimbaji migodi nchini humo, Kaskazini Mashariki mwa Johannesburg uliendelea na kazi kama kawaida.

Zimbabwe inamsaka mshukiwa wa Rwanda

Dalili za mauaji ya kimbari Rwanda
Polisi nchini Zimbabwe, wanasema kuwa wameanzisha msako mkali wa afisaa mmoja mkuu wa zamani nchini Rwanda ambaye anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya Kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda.
Protais Mpiranya alikuwa kamanda wa ulinzi wa rais mwaka huo na anatuhumiwa kwa kuhusika pakubwa na mauaji ya watutsi 800,000 pamoja na wahutu wenye msimamo wa kadri.
Zimbabwe imekuwa ikishutumiwa kwa kumpa hifadhi afisaa huyo wa zamani.
Makama maalum kuhusu mauaji wa kimbari nchini Rwanda imeahidi kumkabidhi zawadi ya dola milioni tano yeyote mwenye taarifa kumhusu Protais.
"Tunamtaka. Awe hai au akiwa amekufa. Tunatafuta taarifa kumhusu ili tumkamate.Hatufahamu mda ambao amekuwa akiishi hapa nchini'' alisema afisaa mkuu wa polisi Zimbabwe Peter Magwenzi.
Mwaka jana afisaa mmoja wa nchi hiyo alikana kuwa Zimbabwe inamhifadhi Protais.

Waasi watawala kimabavu DRC

 

Waasi wa M23
Mkuu wa harakati za kudumisha amani wa Umoja wa mataifa Herve Ladsous ameliambia baraza la usalama la Umoja huo kwamba waasi wameidhinisha kile anachokiita kuwa ni utawala wa kimabavu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Bwana Ladsous amesema waasi wa M23 wanadhibiti idadi kubwa ya maeneo ya Mashariki mwa Congo na wanawatoza kodi wananchi .
 
Umoja wa Mataifa unaishutumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23. Wakati huo huo Maafisa wa Congo wanataka Rwanda iwekewe vikwazo biashara ya madini .
Waziri wa Madini wa Congo, ameziandikia nchi za Marekani na Uingereza akizitolea wito kampuni katika nchi hizo ziache kununua madini kutoka Rwanda, ambayo mengi anasema yanachimbwa katika ardhi ya Congo.
Zaidi ya watu 200,000 wameachwa bila makao kufuatia mapigano Mashariki mwa nchi.
Mkutano wa maafisa wa ngazi ya juu watakaojadili mzozo huo unatarajiwa kufanyika katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa mjini New York wiki ijayo.
"waasi wa M23 wako katika pembe moja ya mkoa wa Kivu Mashariki ambao unapakana na Rwanda na Uganda'' alisema bwana Ladsous wakati akiwahutubia waandishi wa habari mjini New York.
Waasi wanaotoroka vita
"ni kama ambao wanatawala kwani wanawatoza kodi wenyeji wa mkoa huo , jambo hili halikubaliki hata kidogo'' aliongeza bwana Ladsous.
Wakati huohuo, maafisa wa utawala nchini DRC wanataka vikwazo kuwekewa biashara ya madini yanayotoka nchini Rwanda.
Wadadisi wanasema kuwa madini mengi yanayotoka nchini Rwanda huenda yalitoka nchini DRC na kuchimbwa na makundi ya waasi walio na uhusiano na Rwanda.
"namna tunavyoweza kukomesha kabisa mzozo huu ni Rwanda kuwekewa vikwazo vya kibiashara kwa madini yanayotoka nchini humo hadi tutakapoweza kupata suluhu la kudumu kwa mzozo katika mikoa ya Kaskazini na Kusini ma Kivu.'' alisema waziri wa madini wa DRC Martin Kabwelulu. .

Monday, September 10, 2012

LIPUMBA AFUNIKA JANGWANI AUCHAMBUA UCHUMI NA KUTOA MIKAKATI




Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF, Prof.Ibrahim Lipumba akiwasili kwenye Mkutano wa Chama hicho uliofanyika Jangwani jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa chama hicho waliojitokeza kwenye mkutano huo.

Wafuasi wa Chama hicho wakifurahia jambo.
Kikundi cha Mchiriku nacho hakikua mbali kutumbuiza.
Kadi za vyama mbalimbali zilirejeshwa na kukabidhiwa kadi mpya.
Afande Sele nae alitumbuiza kwenye mkutano huo.

Msanii Kala Pina, akitoa burudani kwa wanachama wenzake wa chama hicho, kwenye uchaguzi wa 2010, Kalapina aligombea udiwani kupitia chama hicho kwenye kata ya Kinondoni.