

Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika
eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi


Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini



Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya
kuuwawa kwake

Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na
Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi
ameuwawa katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha
Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo
Mwanahabari huyo Daud
Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku
askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .
Kabla ya kuuwawa kwa
mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa
Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa
haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.
Chanzo cha mwanahabari Mwangosi
kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa
wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu
ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa
kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na
askari mmoja waliaguka chini .
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti
kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka
Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba
cha kuhifadhia maiti .
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika
30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari
matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na
mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.
Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa
vyombo vya habari JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema
limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha
Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria
bila shuruti.
Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi
kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai
viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM)
kuzuia mikutano hiyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael
Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa
habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya
Mufindi.
" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na
wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na
shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote
kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa
"alisisitiza
Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa
kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa
John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya
siasa kwa kipindi hiki cha sensa.
"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa
mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi
kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa
polisi.
Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa
kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa
zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama
vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.
Kamanda Kamuanda alisema kuwa
jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa
kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa
mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali
za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt SlaaWakati jeshi la
polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara
katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama
chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa
lolote litakalojitokeza .
Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya
kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi
zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia
mikutano hiyo tena.
"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho
Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado
kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa
sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5
waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema
hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa
kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.
Pia alisema kuwa kama ni
uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama
ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .
MWISHO